NAIBU WAZIRI SAGINI AMEISHUKURU MAREKANI KUISAIDIA TANZANIA WAKIMBIZI ZAIDI YA 5000
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini ameishukuru nchi ya Marekani kwa kuendelea kufadhili shughuli za hifadhi pamoja na kuipunguzia mzigo Tanzania kuanzia Januari mwaka huu 2023 kwa kuhamisha wakimbizi zaidi ya 5000.
Amesema hayo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini, wakati akifanya mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu Msaidizi wa Ofisi inayoshughulikia Idadi ya Watu, Wakimbizi na Wahamiaji (Bureau of Population, Refugees, and Migration) nchini Marekani Elizabeth H. Campbell.
Aidha, mazungumzo yamefanyika pembeni ya Mkutano wa 74 wa Kamati Tendaji ya UNHCR unaoendelea Geneva, Switzerland ambayo yalihusu hali ya hifadhi ya ukimbizi nchini Tanzania ambapo Sagini "ameshukuru nchi ya Marekani Kwa kuendelea kufadhili shughuli za hifadhi nchini na pamoja na kuipunguzia mzigo Tanzania Kwa kuhamishia nchini Marekani wakimbizi zaidi ya 5000 tangu mwezi January mwaka 2023".
Hivyo, Kwa upande wa Elizabeth, ameeleza kuwa pamoja na kuendelea kuibuka Kwa matukio ya uvunjifu wa amani sehemu mbalimbali duniani , Serikali ya Marekani itaendelea kusaidia eneo hilo la usaidizi wa kibinadamu.
NAIBU WAZIRI SAGINI AMEISHUKURU MAREKANI KUISAIDIA TANZANIA WAKIMBIZI ZAIDI YA 5000
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 12, 2023
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 12, 2023
Rating:




Post a Comment