Waziri Kijaji Aomba Ushirikiano wa WWF Katika Kulinda Mazingira ya Tanzania

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ameliomba Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira naWanyamapori (WWF) liwezeshe jamii kiuchumi kukabili uharibifu wamazingira.
Ametoa ombi hilo Oktoba 30, 2024 alipokutana na kufanya mazungumzo naMkurugenzi Sera na Utetezi wa WWF Dkt. Lin Lin katika kikao cha pembezonimwa Mkutano wa Mkutano wa 16 wa Wakuu wa Nchi wa Uhifadhi waMazingira unaofanyika Cali, Colombia.
Dkt. Kijaji ambaye ameambatana na Ujumbe wa Tanzania, amesisitiza kuwa nimuhimu jamii iwezeshwe kukabiliana na visababishi vya uharibifu wamazingira.
“Kama tunavyofahamu jamii inakabiliwa na changamoto ya kipato cha chinihivyo ni wakati muafaka sasa kwa shirika hili kuwekeza ili wananchi wetuwaweze kukabiliana na athari za uharibifu wa mazingira,” amesema.
Aidha, Mhe. Dkt. Kijaii ametumia nafasi hiyo kupongeza juhudi kubwazinazofanywa na shirika hilo nchini Tanzania katika kuhifadhi mazingira katikamaeneo mbalimbali ya nchi.
Kwa upande wake Dkt. Lin ameipongeza Tanzania kwa kuandaa Shabaha zaKitaifa za Kuhifadhi Bioanuai ambazo zitakuwa na mchango mkubwa katikakupunguza uharibifu wa bioanuai.
Sanjari na hilo pia ametoa pongezi kwa Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi yaMakamu wa Rais kutunga Kanuni za kudhibiti matumizi mifuko ya plastikimwaka 2019 ambazo zinasaidia kukabiliana changamoto ya mifuko ya plastikiiliyopigwa marufuku nchini.
Hata hivyo, Dkt. Lin ameiomba Tanzania kuongeza ushawishi wa kimataifa namsukumo katika majadiliano ya kimataifa yanayoendelea duniani katikakuanzisha Mkataba wa Kimataifa kuhusu udhibiti wa matumizi ya plastiki(Intergovernmental Negotiation Commitee on Plastic, ICNP).
Waziri Dkt. Kijaji yupo nchini Colombia akishiriki Mkutano wa 16 wa Wakuu waNchi wa Uhifadhi wa Mazingira uliofunguliwa Oktoba 21, 2024 na unatarajiwakuhitimishwa Novemba mosi, 2024.
Waziri Kijaji Aomba Ushirikiano wa WWF Katika Kulinda Mazingira ya Tanzania
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 01, 2024
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 01, 2024
Rating:
Post a Comment