Serikali imehimiza kuwa miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini itekelezwe kwa misingi ya uhifadhi, usimamizi wa mazingira na ushirikishwaji wa jamii za wenyeji ili kulinda urithi wa nchi.
Hayo yemesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Fresto Fugange wakati akifungua Kongamano la Wadau wa Mazingira kuhusu Nishati safi aina ya Haidrojeni jijini Dar es Salaam leo Machi 25, 2026.
Kongamano hilo limendaliwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Asasi Binafsi ya
Bora Women Go Green.
Alisema upotevu wa bioanuai ni changamoto kubwa inayohitaji kukabiliana nayo na kwamba dhana kubwa ni kuhakikisha mifumo ikolojia yenye ubora na utajiri wa asili inalindwa.
Dkt. Dugange alieleza kuwa ili kukabiliana na changamoto na athari za mazingira na zile za mabadiliko ya tabianchi, ni lazima kuongeza jitihada za utunzaji na usimamizi wa mazingira, kuwekeza kwenye vyanzo vya nishati mbadala na kuwa na mifumo ya kusaidia kustahimili mabadiliko ya tabianchi.
Licha ya Serikali kuchukua hatua mbalimbali, alisema bado inashuhudiwa changamoto za mazingira katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo aliwahimiza washiriki wa kongamano hilo kujadiliana na kutafakari kwa pamoja ili kubuni mbinu mpya za kuzitatua.
Akipongeza hatua zinazoendelea kuchukuliwa na wadau mbalimbali katika kutekeleza Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia (2024 – 2034), Naibu Waziri huyo alisisitiza kuwa ni lazima kuwa mfano katika kutekeleza sera za kuhimili na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ili kuhakikisha maendeleo endelevu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Katika kongamano hilo, Dkt. Dugange pia alizindua mtambo wa haidrojeni utakaotekelezwa kwa majaribio katika vijiji mbalimbali wilayani Kilwa (Pwani), ambapo alisema kwa Tanzaani hii ni
sehemu ya mapinduzi ya kijani.
“Sote tunatambua maeneo ya Rufiji, Mafia, Kibiti na Kilwa yanajivunia utajiri mkubwa wa bioanuai, hasa mikoko ya pwani na rasilimali za baharini, ambazo zina thamani kubwa kwa mazingira na maisha ya jamii za eneo hilo,“ alisema.
Hivyo, alihimiza kuhakikisha teknolojia hiyo inasambaa nchini ili kulinda mazingira na afya za wananchi akisema kwa kufanya hivyo, tutakuwa tumechangia kwa kiasi kikubwa katika kukabiliana na changamoto kubwa tatu za kidunia, ambazo ni upotevu wa bayoanuai, mabadiliko ya tabia nchi na uchafuzi wa mazigira.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Immaculate Semesi alisema kuna umuhimu wa kuongeza juhudi za kuhamasisha wananchi kutumia nishati safi ya kupikia.
Alisema matumizi ya nishati zisizo safi bado ni changamoto hasa katika maeneo ya vijijini na hivyo kusababisha maradhi na vifo na ndio maana Serikali iliandaa Mkakati wa Matumizi ya Nishati Safi (2024-2030) ili kuhakikksha ifikapo mwaka 2024 30 lenga 80 wanatumia ifikakapo 30.
Dkt. Semesi alisema mkakati huo unalenga kuhakikisha asilimia zaidi ya 80 ya watu wanatumia nishati safi ifikapo mwaka 2030 kwa kuendelea kuwezesha mazingira ya kuwa na uhakika wa matumizi ya gesi, biogesi, majiko janja na teknokojia mbadala rafiki wa mazingira.
“Tumpongeze Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye anatambuliwa kimataifa kama kinara wa nishati safi nchini Tanzania ambayo imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi na leo tunaona juhudi za kuongeza wingi wa vyanzo vya nishati safi,“ alisema.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa ambayo ni wanufaika wa mradi, Mohamed Nyundo alisema mradi huo utasaidia wananchi kuachana matumizi ya nishati chafu ikiwemo kuni na mkaa.
Alisema kwa kuwa wilaya hiyo na Mkoa wa Pwani kwa ujumla umeathiriwa na vitendo vya ukataji miti, mradi huo utakuwa chachu kwa wananchi kuacha vitendo hivyo.
The 2026 AI Wealth Report: Top 5 Ways to Generate Income Using Artificial Intelligence