Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi Aongoza Kilele cha Wiki ya Maji 2026 Mkoani Morogoro
Hotuba ya Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi Kilele cha Wiki ya Maji 2026, Morogoro
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ametoa maagizo mazito kwa Wizara ya Maji na wadau wa maendeleo wakati wa kilele cha Wiki ya Maji Duniani mkoani Morogoro, Machi 22, 2026.
Mambo Muhimu Kutoka Morogoro:
- Ulinzi wa Vyanzo vya Maji: Dkt. Nchimbi amesisitiza umuhimu wa kulinda vyanzo vya maji ili kukabiliana na ongezeko la watu linalokadiriwa kufika milioni 118 ifikapo mwaka 2050.
- Gridi ya Taifa ya Maji: Serikali imedhamiria kuimarisha Gridi ya Taifa ya Maji ili kuondoa kero ya maji kwa wananchi wote, vijijini na mijini.
- Usimamizi wa Mindu Dam: Makamu wa Rais alikagua Bwawa la Mindu na kuzindua mfumo mpya wa kidijitali wa kutabiri mtiririko wa maji mtoni (River Flow Forecasting System).
- Usawa wa Kijinsia: Kaulimbiu ya mwaka huu "Maji na Usawa wa Kijinsia" inalenga kumtua mama ndoo kichwani na kumpunguzia mwanamke adha ya kufuata maji mbali.
Kwa habari zaidi na updates za kila siku, hakikisha unafuatilia biznews.co.tz, chanzo chako namba moja cha habari za biashara na maendeleo Tanzania.
Tags: #DktNchimbi #WikiYaMaji2026 #Morogoro #TanzaniaNews #HabariMpya #Biznews