Ubora Unaoonekana; Benki ya NMB yan'gara tuzo za Euromoney 2026

Benki ya NMB yashinda tuzo tatu za Euromoney 2026 London, ikiimarisha ubora wa huduma, usalama wa fedha na uendelevu Tanzania.
NMB Bank Award
NMB Yatwaa Tuzo Tatu Euromoney 2026 Jijini London
Imechapishwa: Machi 2026 | Mwandishi: Fahadi Msuya

Benki ya NMB imetwaa tuzo tatu katika Tuzo za Euromoney Private Banking 2026 jijini London, ikishinda Benki Bora ya Huduma za Wateja Maalum Tanzania, Benki Salama Zaidi ya Huduma za Wateja Maalum na Benki Bora kwa Uendelevu Tanzania.

Ushindi huo unaendelea kuakisi uimara wa benki hiyo katika kutoa huduma mahususi kwa wateja, kuimarisha usalama wa fedha na kuongoza katika utekelezaji wa mikakati ya fedha endelevu.

Mafanikio haya yanaendelea kuimarisha nafasi ya Benki ya NMB kama kinara wa ubunifu na mshirika wa maendeleo ya uchumi Tanzania na kanda ya Afrika Mashariki.

NextGen Digital... Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...