Header AD

header ads

WAZIRI KAIRUKI ASHIRIKI MISA YA KUMBUKIZI YA MIAKA 23 YA BABA WA TAIFA








Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki ameungana na Familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kushiriki Misa Maalum ya Kumuombea aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage ikiwa ni kumbukizi ya Miaka 23 ya Kifo chake.


Misa hiyo imehudhuliwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango.

Ibada ya Misa imefanyika Leo tarehe 14 Oktoba 2022 katika kanisa kuu katoliki  Bukoba Mjini mkoani Kagera na kuongozwa na Mhashamu Askofu Method Kilaini ambaye ni Askofu Msaidizi Jimbo Katoliki la Bukoba



WAZIRI KAIRUKI ASHIRIKI MISA YA KUMBUKIZI YA MIAKA 23 YA BABA WA TAIFA WAZIRI KAIRUKI ASHIRIKI MISA YA KUMBUKIZI YA MIAKA 23 YA BABA WA TAIFA Reviewed by Fahadi Msuya on October 14, 2022 Rating: 5