Header AD

header ads

KITUO CHA NYUMBA YA FURAHA CHAOMBA MSAADA KWA WADAU



Na Hadija Bagasha Tanga, 

Kituo cha nyumba ya furaha kinacholea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu kimeomba msaada kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo Mkoani ili kiweze kujiendesha na kusaidia jamii inayoishi kwenye mazingira hatarishi. 

Mlezi wa kituo hicho Irene Augustino ameyasema hayo wakati akipokea msaada wa vyakula,  fedha,  na vifaa mbalimbali kutoka kwa shirikisho la michezo kutoka Wizara,  Idara na taasisi za Serikali (SHIMIWI)  amesema kuwa kituo  hicho kwa sasa kina jumla ya watoto 70 ambao wanahitaji msaada na kwamba kwa sasa kinajikuta kwenye wakati mgumu kutokana na ukosefu wa wafadhili. 


Mlezi wa kituo hicho amesema lengo kuu la kuwalea watoto hao ni kuokoa maisha yao kwani watoto wanaowalea ni zaidi ya yatima sababu hawana hata utegemezi wa ndugu yeyote huku wengine wakitoka kwenye mazingira hatarishi. 

"Kituo chetu hakina mfadhili yeyote zaidi ya mtu mwenye mapenzi mema kwahiyo kwa njia ya ujio wenu tunashukuru kwani mmekuwa wafadhili wakubwa leo hii wa kituo chetu na watoto hawa tunawapata kutoka ustawi wa jamii hatuchukui watoto kiholela holela, "Alisema sister Irene. 

Aliongeza kuwa tunapoona mnaguswa na historia ya maisha yetu ya kuwahudumia watoto tunafurahi na kufarijika sanaa hata nyinyi mmeona mlivyokuwa mnaingia watoto walikuwa wanaonyesha furaha kuonyesha ni jinsi gani wazazi wanawaunga mkono. 

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada kwenye kituo hicho Katibu wa shirikisho la michezo kutoka Wizara, idara na Taasisi za Serikali (SHIMIWI) Alex Temba amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kuona jamii hiyo ina uhitaji wa misaada kutoka kwa jamii. 


Temba amesema kuwa watumishi ambao ni wana Shimiwi wameona ni vyema kurudisha furaha na kile ambacho serikali imewapa kwenye vituo mbalimbali kama fadhila kwao. 

"Kipekee wanashimiwi wanamshukuru Rais Samia kwa kurudisha michezo hii na sisi tunamuahidi siki zote popote tutakapokwenda kipekee tutatenga siku maalumu kwajili ya kurudisha kile ambacho serikali imetupa kwajili ya watu wenye mahitaji mbalimbali, "alisema Temba. 

Aidha Temba amesema gharama za fedha ambazo timu 67 zilizoshiriki michezo hiyo mwaka 2022 ni zaidi ya shilingi milioni 4 pamoja na vifaa mbalimbali ikiwemo vyakula. 


"Tumependa kuienzi siku hii tumebahatika kufanya michezo yetu ambayo imegongana na siku ya kumkumbuka baba wa Taifa tukaona siku hii tusiiweke tukio lolote la kimichezo ili watumishi waweze kupata nafasi ya kutembelea sehemu mbalimbali ambazo zinahitaji sisi kama wanadamu kurudisha fadhila zetu kwao, "alisisitiza Temba. 

Katika kuthamini jamii inayoishii kwenye mazingira magumu shirikisho la michezo kutoka Wizara,  Idara na Taasisi za serikali (SHIMIWI) limetoa misaada mbalimbali kwenye jamii inayoishi kwenye mazingira magumu ikiwemo  kituo cha wazee wasiojiweza,  chuo cha walemavu Masiwani, na kituo cha watoto yatima cha Nyumba ya furaha. 


Msaada uliotolewa ni pamoja na fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 1 kwa kila kituo,  Vyakula,  mafuta,  sambamba na vifaa vya shule kwa wanafunzi,  mchango wanaoutoa kuadhimisha kifo cha Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere. 



KITUO CHA NYUMBA YA FURAHA CHAOMBA MSAADA KWA WADAU KITUO CHA NYUMBA YA FURAHA CHAOMBA MSAADA KWA WADAU Reviewed by Fahadi Msuya on October 14, 2022 Rating: 5