WAZIRI KAIRUKI AWAKABIDHI VITENDEA KAZI WAKUU WA MIKOA YA SONGWE NA SHINYANGA
NA OR-TAMISEMI
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah ,Mtumba jijini Dodoma amekutana na kuzungumza na wakuu wa mikoa wapya na kuwakabidhi vitendea kazi.
Wakuu wa mikoa hao ni Mhe. Dkt. Francis K. Michael ambaye ni Mkuu wa Mkoa Songwe na Mhe. Christina S. Mndeme Mkuu wa Mkoa Shinyanga .
Waziri Kairuki amewata wakuu waikoa hao kutekeleza kikamilifu majukumu yao ili kutimiza azma ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwaamini ili kumwakilisha katika mikoa hiyo.
Aidha, Waziri Kairuki amewataka wakuu wa mikoa kushirikiana na watendaji wote katika maeneo yao ili kuhakikisha kipaumbele cha Serikali kinachukua nafasi ya kwanza ili kuendana na utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Pia amewataka kujikita kutatua kero za wananchi katika maeneo yapo mara zinapojitokeza au kuwasilisha kwenye mamlaka husika ili ziweke kutafutiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.
WAZIRI KAIRUKI AWAKABIDHI VITENDEA KAZI WAKUU WA MIKOA YA SONGWE NA SHINYANGA
Reviewed by Fahadi Msuya
on
March 01, 2023
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
March 01, 2023
Rating:


Post a Comment